Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli wapatiwa vishikwambi.
Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri kwa mwaka wafedha 2023/2024 imenunua vishikwambi (Tablets) 24 kwa Waheshimiwa Madiwani na vishikwambi (tablets) 18 za Menejiment vyenye thamani ya shilingi milioni 10.5.
Mkurugenzi Mtendaji Ndugu, Baraka Zikatimu alieleza kuwa vishikwambi hivyo vimenunuliwa ikiwa ni utekelezaji wa azimio la baraza la madiwani kwa bajeti ya mwaka 2023/24 ambapo iliazimiwa kununua vishikwambi hivyo kwa ajili ya Waheshimiwa Madiwani na Menejimenti ili kuondokana na matumizi makubwa ya karatasi, kuokoa gharama na hivyo kuelekeza fedha hizo kwenye shughuli za kimaendeleo pamoja na kuendesha vikao vyote kidigitali.
Tukio hilo la kukabidhiwa vishikwambi lilifanyika tarehe 06 Februari, 2024 katika ukumbi Mkubwa wa Halmashauri ambapo maelekezo ya namba ya kuvitumia vishikwambi hivyo wakati wa kutuma taarifa na wakati wa vikao yalitolewa kwa madiwani na wataalam wa Halmashauri.
Akikabidhi vishikwambi hivyo kwa Waheshimiwa Madiwani na Watendaji Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Amiri A. Sheiza awaliwaomba wavitunze kwani ni vitendea kazi muhimu katika kazi na vitatumika kupokelea taarifa mbalimbali za halmashauri kwa kamati zote za kudumu na mkutano wa baraza la madiwani.
Akitoa shukrani Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bumbuli Mhe. Hozza A. Mandia Diwani wa kata ya Kwemkomole kwa niaba ya Waheshimiwa Madiwani, alimshukuru Mkurugenzi Mtendaji na Menejimenti kwa kutekeleza azimio hilo kwa vitendo na kuomba utekelezaji wa maazimio mengine ya baraza uendelee kwa vitendo.
02 KITONGOJI CHA UGUNGA
Postal Address: S.L.P 111, BUMBULI
Telephone: 0272977530
Mobile:
Email: ded@bumbuklidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli. Haki Zote Zimehifadhiwa.