Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli Mhe. Amiri A. Sheiza leo tarehe 04 Septemba, 2023 amepokea na kukabidhi vifaa kwa wakulima na wajasiliamali wa vikundi vinne vilivyopo katika kata ya mamba na mayo.
Vifaa hivyo ni pamoja na Maguta (toyo), mashine ya kufyatulia tofali za kisasa, pampu ya maji, viriba, keni pamoja na paipu ya kuvutia maji. Vifaa hivyo vimetolewa na shirika la “CARE International” ambalo linalojishughulisha na kuwajengea uwezo wakulima na wajasiliamali katika kukuza fursa za kiuchumi ili kuongeza tija katika ubora, viwango vya uzalishaji.
Akiongea katika hafla hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri amesema “Anaishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kuendeleza sekta ya kilimo kupitia fursa mbalimbali anazo zitoa, pia anaishukuru taasisi ya CARE kwa kutoa vifaa ambavyo vitawasaidia wakulima na wajasiliamali hao katika shughuli zao. Aidha aliwataka wakulima na wajasiliamali waliopata vifaa hivyo kuvitumia vizuri ili viweze kuwaletea tija na kuwaongezea vipato na kuwa mabalozi wazuri kwa wenzao.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli Ndugu Baraka M. Zikatimu amesema, anaishukuru na kuipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kuweka sera, miongozo mbalimbali inayotoa fursa kwa wadau wa maendeleo kushirikiana na serikali kuleta maendeleo kwa amani na utulivu
Wawakilishi wa Taasisi ya CARE International Ndugu Barnabas Mtelevu meneja wa mradi na Bi. Neema Lweeka mratibu wa mradi wameishukuru Serikali kwa kuwaamini na kuwapatia nafasi ya kuisaidia jamii katika kuwapatia fursa mbalimbali ambazo zimeisaidia serikali katika kuleta maendeleo ya wananchi na Taifa.
02 KITONGOJI CHA UGUNGA
Postal Address: S.L.P 111, BUMBULI
Telephone: 0272977530
Mobile:
Email: ded@bumbuklidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli. Haki Zote Zimehifadhiwa.