Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua jengo jipya la Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli, mkoani Tanga, ambalo ujenzi wake umegharimu Shilingi za Kitanzania Bilioni 5.5.
Mhe. Rais amezindua jengo hilo leo tarehe 24 Februari, 2025 na baada ya kuzindua jengo hilo, Rais Samia ameeleza furaha yake kwa mapokezi mazuri ya wananchi wa Bumbuli.
Mhe. Rais amewashukuru Wakandarasi, Wataalam washauri na wasimamizi wa mradi, na Wafanyakazi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli kwa jitihada zao katika kuhakikisha jengo linakamilika kwa wakati na ubora.
Kwa upande mwengine Mhe. Samia ameeleza dhamira na lengo la ujenzi wa jengo hilo kuwa ni kuhakikisha watumishi wa Halmashauri wanafanya kazi katika mazingira bora na wananchi wanapata huduma kwa urahisi.
“Jengo hili ni lenu wananchi wa Bumbuli naomba mlitumie kwa kupata huduma, watumishi wote kwa sasa wapo katika jengo hili hivyo mje mpate huduma hapa, na naomba mlitumie kwa manufaa yenu. Lengo letu ni kuboresha huduma kwa wananchi na kutoa fursa kwa watumishi wetu kufanya kazi zao katika mazingira bora na kwa ufanisi,” amesema Rais Samia.
02 KITONGOJI CHA UGUNGA
Postal Address: S.L.P 111, BUMBULI
Telephone: 0272977530
Mobile:
Email: ded@bumbuklidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli. Haki Zote Zimehifadhiwa.