Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli katika kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wake imetekeleza mradi wa ujenzi wa jengo lake la utawala. Jengo hilo lina vyumba 72 vya watumishi na Wakuu wa Divisheni na Vitengo vyote vya Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli.
Jengo hilo limejengwa kwa lengo la kuhakikisha watumishi wa Halmashauri wanafanya kazi katika mazingira bora na wananchi wanapata huduma kwa urahisi.
Gharama za ujenzi wa jengo hilo ni Shilingi za Kitanzania Bilioni 5.5 fedha kutoka Serikali Kuu, na kukamilika kwa ujenzi wa jengo hilo limesaidia kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
02 KITONGOJI CHA UGUNGA
Postal Address: S.L.P 111, BUMBULI
Telephone: 0272977530
Mobile:
Email: ded@bumbuklidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli. Haki Zote Zimehifadhiwa.