Timu za wataalamu kutoka ngazi ya Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa wanaosimamia utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ya awali na msingi "BOOST" kutoka mikoa miwili ya Tanga na Kilimanjaro wamepewa mafunzo elekezi kwa lengo la kujengewa uwezo kuhusu usimamizi wa mradi wa BOOST.
Mafunzo kazi hayo ya siku mbili ambayo yameandaliwa na OR-TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuanzia tarehe 16 hadi 17 Disemba, 2022 yamefanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Wasichana Korogwe na kuhudhuriwa na wajumbe wa timu za usimamizi kutoka katika Halmashauri za Mikoa husika.
Katika mafunzo kazi hayo Afua nane ziliwasilishwa ambazo ni :-
Aidha, lengo la mafunzo haya ni kuhakikisha na kuweka msisitizo kwa timu hizi kuhakikisha usimamizi wa mahitaji ya msingi na utekelezaji wa Afua unakamilishwa ili kukidhi vigezo vya kupata msaada wa kifedha kutoka Benki ya Dunia zitakazowezesha kupunguza na kuondoa changamoto mbalimbali za kielimu katika eneo la kujifunzaji na ufundishaji.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini:
Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli
02 KITONGOJI CHA UGUNGA
Postal Address: S.L.P 111, BUMBULI
Telephone: 0272977530
Mobile:
Email: ded@bumbuklidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli. Haki Zote Zimehifadhiwa.