Divisheni ya Elimu ya Sekondari yafanya kikao kazi cha tathmini ya vigezo vya uendaji kazi (KPI) na utoaji wa tuzo kwa walimu na wanafunzi waliofanya vyema, tukio lililofanyika tarehe 22.03.2023 katika ukumbi wa shule ya Sekondari Mbelei
Kikao hicho kilihudhuriwa na Wakuu wa shule 29 za Sekondari za serikali na binafsi, Maafisa Elimu Kata 18, pamoja na Maafisa kutoka divisheni ya Sekondari. Mgeni Rasmi alikuwa ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bumbuli Mhe. Amiri Shehiza akiambata na Kaimu Mkurugenzi Bw. Netson Masaki.
Aidha, tathimini ya matokeo ya kidato cha nne na upimaji kidato cha pili iliainishwa kwa kipindi cha miaka 3 mfululizo 2020-2022 ambapo ilionesha katika kipindi hicho hali ya ufaulu wa kidato cha nne imekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka na kuiwezesha Halmashauri ya Bumbuli kushika nafasi ya tatu kimkoa wakati kidato cha pili hali si nzuri ambapo ufaulu umeshuka kwa asilimia 5.5 ukilinganisha na matokeo ya 2021.
Akiongea na Maafisa hao Mwenyekiti wa Halmashauri amesema "anawapongeza walimu kwa jitihada wanazozionesha katika kuongeza juhudi za ufundishaji na upandishaji ufaulu wanafunzi, kuwa wavumilivu, kujitoa na kuwa waadilifu kwa kutoa huduma bora "
Afisa Elimu Sekondari Bw. John Mmbaga amesema katika kuongeza ufaulu Idara imeweka mikakati mbalimbali ambayo ni ufuatiliaji wa ufundishaji na ujifunzaji, kutoa mazoezi na mitihani ya upimaji mara kwa mara, vikao vya tathmini, msawazo wa walimu, kufuatilia utekelezaji wa mikataba ya utendaji kazi na kuisimamia, kuelimisha wazazi/walezi kushiriki na kutimiza wajibu wao wa kutoa chakula kwa watoto, kuthibiti utoro. Pamoja na hayo yote amesisitiza kuendelea kusimamia na kutoa mafunzo rekebishi kwa waalimu.
Aidha, Halmashauri ya Bumbuli inaishukuru Serikali ya awamu ya 6 kwa kuboresha miundombinu ya shule, kwa mwaka 2022/23 madarasa yamejengwa 64 umaliziaji wa madarasa 3 na Maabara 5.
KAZI IENDELEE!!!
02 KITONGOJI CHA UGUNGA
Postal Address: S.L.P 111, BUMBULI
Telephone: 0272977530
Mobile:
Email: ded@bumbuklidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli. Haki Zote Zimehifadhiwa.