Uvunaji wa Miti ya kupandwa ya Mbao
1. Muombaji anayetaka kuvuna miti ya kupandwa ya mbao atalazimika kuandika barua yake ya kusudio la kufanya hivyo kwenda kwa Halmashauri ya Kijiji husika ikitaja aina ya uvunaji kama vile mbao, magogo, mirunda, mahali uvunaji huo utakapofanyika, madhumuni ya uvunaji, aina ya miti na idadi yake.
2. Halmashauri ya Kijiji husika ikikubali ombi hilo, baada ya kupata ushauri wa Kamati ya Mazingira ya Kijiji, italipitisha ombi hilo kwa kuandika barua kwenda kwa Afisa Misitu Wilaya akiambatanisha na barua ya muombaji wa uvunaji huo.
3. Afisa Misitu Wilaya akikubali maombi hayo ya uvunaji, atayapitisha na kisha muombaji atapewa Ruhusa ya Uvunaji wa Mazao Hayo kwa kujaza Fomu Na. 1
4. Muombaji aliyepewa ruhusa ya uvunaji ataendelea na kazi yake na atakapomaliza atatakiwa kupata barua ya Mtendaji wa Kijiji husika kwenda kwa Afisa Misitu Wilaya, ikimtaarifu kuwa kazi ya uvunaji imekamilika na kunahitajika Huduma ya Nyundo na Kibali cha Kusafirishia mazao hayo kwa sasa.
5. Afisa Misitu Wilaya akishapokea barua hiyo atamuelekeza Meneja Misitu Wilaya wa TFS kutoa huduma hizo kwa mvunaji husika.
6. Mvunaji husika atalazimika kulipa ushuru wa Halmashauri ya Wilaya, gharama za kibali cha kusafirisia mazao ya misitu, faini ya Kutumia Msumeno wa Nyororo kabla ya kupata huduma husika.
7. Wakati wa kugongewa Nyundo, Mvunaji, Bwana Miti na Mtendaji wa Kijiji watalazimika kujaza Fomu Na. 2 ya Ruhusa ya Kusafirisha Mazao ya Misitu ambayo ni moja ya nyaraka muhimu.
Uvunaji wa Miti ya Matunda
1. Muombaji anayetaka kuvuna miti ya matunda atalazimika kuandika barua yake ya kusudio la kufanya hivyo kwenda kwa Halmashauri ya Kijiji husika ikitaja aina ya uvunaji kama vile mbao, magogo, mirunda, mahali uvunaji huo utakapofanyika, madhumuni ya uvunaji, aina ya miti na idadi yake.
2. Halmashauri ya Kijiji husika ikikubali ombi hilo, baada ya kupata ushauri wa Bwana au Bibi shamba na Kamati ya Mazingira ya Kijiji, italipitisha ombi hilo kwa kuandika barua kwenda kwa Afisa Misitu Wilaya akiambatanisha na barua ya muombaji wa uvunaji huo.
3. Afisa Misitu Wilaya akikubali maombi hayo ya uvunaji, atayapitisha na kisha muombaji atapewa Ruhusa ya Uvunaji wa Mazao Hayo kwa Kujaza Fomu Namba Moja.
4. Muombaji aliyepewa ruhusa ya uvunaji ataendelea na kazi yake na atakapomaliza atatakiwa kupata barua ya Mtendaji wa Kijiji husika kwenda kwa Afisa Misitu Wilaya, ikimtaarifu kuwa kazi ya uvunaji imekamilika na kunahitajika Huduma ya Nyundo na Kibali cha Kusafirishia mazao hayo kwa sasa.
5. Afisa Misitu Wilaya akishapokea barua hiyo atamuelekeza Meneja Misitu Wilaya wa TFS kutoa huduma hizo kwa mvunaji husika.
6. Mvunaji husika atalazimika kulipa Ushuru wa Halmashauri ya Wilaya, Gharama za Kibali cha Kusafirisia Mazao ya Misitu, Faini ya Kutumia Msumeno wa Nyororo kabla ya kupata huduma husika.
7. Wakati wa Kugongewa Nyundo, Mvunaji, Bwana Miti na Mtendaji wa Kijiji watalazimika kujaza Fomu Namba Mbili ya Ruhusa ya Kusafirisha Mazao ya Misitu ambayo ni moja ya nyaraka muhimu.
Uvunaji wa Miti ya asili
1. Muombaji anayetaka kuvuna miti ya miti ya asili atalazimika kuandika barua yake ya kusudio la kufanya hivyo kwenda kwa Halmashauri ya Kijiji husika ikitaja aina ya uvunaji kama vile mbao, magogo au mirunda, mahali uvunaji huo utakapofanyika, madhumuni ya uvunaji, aina ya miti na idadi yake.
2. Halmashauri ya Kijiji husika ikikubali ombi hilo, baada ya kupata ushauri wa Kamati ya Mazingira ya Kijiji, italipitisha ombi hilo kwa kuandika muhtasari kwenda kwa Afisa Misitu Wilaya akiambatanisha na barua ya muombaji wa uvunaji huo.
3. Afisa Misitu Wilaya akishayapokea maombi hayo ya uvunaji, atayawasilisha kwenye Kamati ya Uvunaji Wilaya ambako yatajadiliwa rasmi.
4. Maombi hayo yakishapitishwa, ukaguzi na upimaji wa miti hiyo utafaanyika ili kukadiria ujazo na gharama za malipo, kisha waombaji watapewa Liseni ya Uvunaji na Ruhusa ya Uvunaji wa Mazao Hayo kwa Kujaza Fomu Namba Moja.
5. Muombaji aliyepewa Liseni na ruhusa ya uvunaji ataendelea na kazi yake na atakapomaliza atatakiwa kupata barua ya Mtendaji wa Kijiji husika kwenda kwa Afisa Misitu Wilaya, ikimtaarifu kuwa kazi ya uvunaji imekamilika na kunahitajika Huduma ya Nyundo na Kibali cha Kusafirishia (TP) mazao hayo kwa sasa.
6. Afisa Misitu Wilaya akishapokea barua hiyo atamuelekeza Meneja Misitu Wilaya wa TFS kutoa huduma hizo kwa mvunaji husika.
7. Mvunaji husika atalazimika kulipa Ushuru wa Halmashauri ya Wilaya, Gharama za Kibali cha Kusafirisia Mazao ya Misitu, Faini ya Kutumia Msumeno wa Nyororo kabla ya kupata huduma husika.
8. Wakati wa Kugongewa Nyundo, Mvunaji, Bwana Miti na Mtendaji wa Kijiji watalazimika kujaza Fomu Namba Mbili ya Ruhusa ya Kusafirisha Mazao ya Misitu ambayo ni moja ya nyaraka muhimu.
02 KITONGOJI CHA UGUNGA
Postal Address: S.L.P 111, BUMBULI
Telephone: 0272977530
Mobile:
Email: ded@bumbuklidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli. Haki Zote Zimehifadhiwa.