Mimi, Mwenyekiti wa Halmashauri ninakukaribisha katika tovuti rasmi ya Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli ambapo tunaamini kuwa wananchi, wadau wa maendeleo, wawekezaji, watalii na wageni mbalimbali wanapata taarifa za kuaminika za mipango na mikakati ya utoaji huduma bora za kijamii na kiuchumi kwa kutumia rasilimali zilizopo kwa ufanisi na kuzingatia utawala bora kwa ustawi na maisha bora ya jamii na wadau mbalimbali wa Halmashauri.
Upatikanaji na utoaji wa taarifa ni takwa la Kisheria kama inavyoelezwa katika Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tunajivunia Halmashauri yetu na huduma mbalimbali tunazotoa kwa wananchi wetu na wadau mbalimbali. Tunashukuru kwa kutembelea tovuti yetu na tunaamini kuwa umenufaika kwa taarifa mbalimbali za utekelezaji Serikalini, na kukuhakikishia kuwa tutaendelea kuboresha na kuhuisha tovuti hii kwa taarifa mbalimbali kadri muda unavyokwenda ili kukidhi matarajio yako kwa ubora wa hali ya juu.
juu.
02 KITONGOJI CHA UGUNGA
Postal Address: S.L.P 111, BUMBULI
Telephone: 0272977530
Mobile:
Email: ded@bumbuklidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli. Haki Zote Zimehifadhiwa.